• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mazungumzo ni njia pekee ya kutatua mkwaruzano wa biashara kati ya China na Marekani

    (GMT+08:00) 2018-09-18 16:49:37

    Marekani imetangaza kuongeza ushuru wa forodha kwa bidhaa kutoka China zenye thamani ya dola bilioni 200 za Kimarekani kuanzia tarehe 24 mwezi huu. Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang amesema, mazungumzo ni njia sahihi pekee ya kutatua mkwaruzano wa biashara kati ya China na Marekani, lakini hadi sasa vitendo vya Marekani havijaonesha udhati wake.

    Bw.Geng amesema, China italazimika kujibu hatua hii ya Marekani, ili kulinda maslahi yake halali, na utaratibu huria wa biashara duniani. Marekani kuongeza ushuru wa forodha wa bidhaa kutoka China pia kumeleta utatanishi mpya kwa mazungumzo kati ya nchi hizo mbili. China imefafanua msimamo wake kuhusu suala hilo mara nyingi, na kusisitiza kuwa mazungumzo yanayofanywa juu ya msingi wa usawa, uaminifu na kuheshimiana ni njia sahihi pekee ya kutatua mkwaruzano wa biashara.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako