• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yatoa kauli kuhusu uamuzi wa Marekani wa kuongeza ushuru kwa bidhaa za China zenye thamani ya dola bilioni 200 za Kimarekani

    (GMT+08:00) 2018-09-18 18:59:54

    Wizara ya Biashara ya China leo imetoa kauli kuhusu uamuzi wa Marekani wa kuongeza ushuru kwa bidhaa za China zenye thamani ya dola za Kimarekani bilioni 200.

    Msemaji wa Wizara hiyo Gao Feng amesema, Marekani, bila kujali upinzani kutoka ndani na nje ya nchi hiyo, imetoa tangazo la kuongeza asilimia 10 zaidi ya kodi kwenye bidhaa za China kuanzia tarehe 24 mwezi huu. Amesema China imesikitishwa sana na uamuzi huo, na kwamba italazimika kuchukua hatua za kujibu ili kulinda haki na maslahi yake halali, na pia kulinda biashara huria ya kimataifa.

    Amesema China inatarajia kuwa Marekani itatambua athari mbaya zinazoweza kujitokeza kutokana na kitendo hicho na kufanya marekebisho kwa muda mwafaka na kwa njia za kuaminika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako