• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Wakulima wa korosho walenga kuuza tani 2,000

    (GMT+08:00) 2018-09-18 19:14:07
    Wadau wa korosho mkoani Tanga, wamejiwekea mikakati ya kufanyia kazi changamoto zinazokwaza uzalishaji na ununuzi wa zao hilo ili msimu ujao ununuzi ufikie tani 2,000 kutoka tani 734 mwaka 2017/18.

    Mikakati hiyo iliwekwa juzi katika kikao kilichoandaliwa na Bodi ya Korosho Tanzania (CBT) na kuhudhuriwa na wakulima, wanunuzi na viongozi wa halmashauri zote za Tanga.

    Miongoni mwa changamoto zilizotajwa ni kuchelewa kufunga minada ya ununuzi hivyo kutoa nafasi kwa walanguzi kununua nje ya mfumo rasmi kisha kuzitorosha nje ya nchi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako