• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kongamano la haki za binadamu la mwaka 2018 lafanyika Beijing

    (GMT+08:00) 2018-09-18 19:14:33

    Kongamano la haki za binadamu la mwaka 2018 limefanyika leo hapa Beijing na kufunguliwa rasmi na mjumbe wa ofisi ya siasa ya kamati kuu ya chama cha kikomunisti cha China Bw. Huang Kunming.

    Katika hotuba yake, Bw. Huang Kunming amesema kutimiza na kuwa na haki za binadamu ni lengo la binadamu wote duniani, na kuheshimu na kuhakikisha haki za binadamu ni msimamo na utetezi wa Chama cha Kikomunisti cha China na serikali ya China. Katika miaka 40 iliyopita tangu China ifanye mageuzi na kufungua mlango, masuala ya haki za binadamu ya China yamepata maendeleo makubwa, na nchini China haki hizo zinatimizwa kidhahiri.

    Ameongeza kuwa, kundoa umaskini ni haki ya kimsingi ya watu wa nchi mbalimbali wanaotaka maisha mazuri, na China siku zote inapendekeza na kuhimiza kazi za kupunguza umaskini duniani. Pia China inapenda kushirikiana na pande mbalimbali za dunia kufanya juhudi katika kuondoa umaskini, kuhakikisha haki za binadamu na kushirikiana kujenga jumuiya yenye mustakabali wa pamoja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako