• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Algeria: Algeria na China kujenga kiwanda cha phosphate

    (GMT+08:00) 2018-09-18 19:14:46
    Algeria na China zitashirikiana kujenga kiwanda cha madini ya phosphate kwa garama ya dola bilioni 6 katika eneo la kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.

    Waziri wa viwanda na madini Youcef Yousfi,amesema mradi huo unalenga kusaidia nchi hiyo kuanza kuzalisha bidhaa za madini hayo kama vile mbolea.

    Ushirikiano huo utakuwa kati ya kampuni mbili za Algeria Sonatrach na Semidal-Manal, na mbili za China CITIC na Wengfu Group.

    Mgao wa China kwenye mradi huo ni asilimia 49 huku Algeria ikimiliki mgao mkubwa wa asilimia 51.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako