• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Zimbabwe apitisha bajeti ya dola za kimarekani milioni 64 kupambana na kipindupindu

    (GMT+08:00) 2018-09-19 19:27:05

    Rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe amepitisha bajeti ya dola za kimarekani milioni 64 zinazohitajika haraka katika kupambana na mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu ambao mpaka sasa umesababisha vifo vya watu 30 mjini Harare.

    Mwenyekiti wa kamati ya Baraza la mawaziri inayoshughulikia usimamizi wa majanga July Moyo amesema, fedha hizo pia zitatumika kupambana na homa ya matumbo ambayo pia imelikumba jiji la Harare na sehemu nyingine nchini humo. Amesema serikali imechukua hatua hiyo baada ya rais Mnangagwa kutangaza mlipuko wa kipindupindu kama janga la taifa tarehe 12 mwezi huu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako