• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Waziri mkuu wa China asisitiza kuongeza nguvu ya kusukuma mbele kufungua mlango na kulegeza uthibiti wa kuingia katika soko

  (GMT+08:00) 2018-09-19 20:20:51

  Mkutano wa mwaka 2018 wa waongozaji wapya wa Baraza la Uchumi la Dunia, ambao pia ni mkutano wa 12 wa majira ya joto wa Davos umefunguliwa leo huko Tianjin. Akihutubia ufunguzi wa mkutano huo, Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang amesema, China inapaswa kuongeza nguvu ya kusukuma mbele kufungua mlango, kuzidisha mageuzi, kulegeza zaidi uthibiti wa kuingia katika soko, kuongeza wazi wa sera, na kutekeleza usimamizi wenye haki na usawa.

  Kauli mbiu ya mkutano huo ni "kujenga jamii yenye uvumbuzi katika mageuzi ya nne ya kiviwanda", na umehudhuriwa na wajumbe wapatao 2,300 kutoka nchi zaidi 100. Katika hotuba yake, waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang amesema, kwa sasa sekta ya teknolojia ya juu na sekta ya utengenezaji wa kisasa zinaongoza maendeleo ya viwanda, sekta ya huduma imetoa aina mpya na mifumo mipya, na miundo ya viwanda imeboreshwa kwa kasi. Nguvu mpya zimechangia kwa zaidi ya theluthi moja katika ongezeko la uchumi, na zimeweke msingi imara kwa ajili ya maendeleo mazuri na ya kudumu ya uchumi.

  "Katika nusu ya kwanza ya mwaka huu, ongezeko la uchumi wa China limefikia asilimia 6.8, ambayo imekuwa kati ya asilimia 6.7 hadi 6.9 kwa miezi 36. Katika miezi minane ya kwanza ya mwaka huu, watu zaidi ya milioni 10 mijini wamepata ajira, kiasi cha watu wanaopoteza ajira ni karibu asilimia 5, ambacho ni kiwango cha chini katika historia. Kwa ujumla, uchumi wa China umedumisha maendeleo yenye utulivu, hasa nguvu mpya ya maendeleo inaongezeka. "

  Bw. Li Keqiang amesema, katika miaka kadhaa iliyopita, serikali ya China imefanya juhudi katika kuhimiza kurahisisha utawala, kupunguza ushuru na ada, kupunguza kwa ufanisi gharama za biashara na gharama za uzalishaji za viwanda, na kuhimiza kuboresha mazingira ya biashara na kuinua ufanisi wa viwanda. Katika siku za mbele, China itaongeza juhudi katika kupunguza ushuru na ada.

  "Tutaongeza nguvu ya kupunguza ushuru na ada, kwa sasa siyo tu tunatekeleza sera zilizotolewa za kupunguza ushuru, na kukataa kithabiti kuongeza mizigo mpya kwa viwanda, pia tutachunguza sera za kupunguza ushuru na ada kwa kiasi kikubwa. Sera hizo ni sawa kwa makampuni ya China na nchi za nje yanayosajiliwa nchini China. Pia tutaboresha mazingira ya kufanya biashara, kupitia sera za kurahisisha utawala na usimamizi wa usawa, kupanua uthibiti wa kuingia katika soko, ili makampuni yenye mitaji ya nje yana ushindani wa usawa katika soko la China. "

  Kwenye hotuba yake, Li Keqiang pia ameeleza hatua za China za kupanua kufungua mlango na kusisitiza kuwa, uchumi wa China umekua kutokana na kufungua mlango. Mwaka huu China imelegeza kwa kiasi kikubwa uthibiti wa kuingia soko kwa sekta ya huduma, hasa kwa mambo ya fedha, sera hizo zinaharakisha kutekelezwa. Wakati huo huo, China itapunguza zaidi ushuru wa bidhaa kutoka nje.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako