• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yalalamikia hatua ya Marekani ya kuongeza ushuru wa bidhaa huku idai kufanya mazungumzo

    (GMT+08:00) 2018-09-19 20:59:57

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang amesema, Marekani inapanga kuongeza ushuru wa bidhaa zinazotoka China huku idai kutaka kufanya mazungumzo.

    Jana, Marekani ilitangaza kuongeza ushuru wa forodha kwa bidhaa kutoka China zenye thamani ya dola bilioni 200 za Kimarekani, huku Waziri wa biashara wa Marekani akisema kuwa, madhumuni ya nchi hiyo ni kufanya mazungumzo ya kiujenzi na China ili kutatua mvutano huo.

    Bw. Geng amesisitiza kuwa matishio ya Marekani dhidi ya China hayatafanya kazi, China itaendelea kulinda maslahi yake halali. Amesema China inaona ushirikiano wa uchumi na biashara unanufaisha pande zote mbili, na mazungumzo ni njia pekee iliyo sahihi katika kutatua mvutano wa biashara kati ya nchi hizo mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako