• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya yaandaa matembezi ya umma ili kuongeza ufuatiliaji wa shida za wakimbizi wa Afrika

    (GMT+08:00) 2018-09-20 09:19:34

    Matembezi ya umma yatafanyika Jumapili jijini Nairobi ili kuongeza ufahamu kuhusu shida zinazowakabili wakimbizi wa Afrika kutokana na changamoto mbalimbali ukiwemo umaskini na kutengana na jamii.

    Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR limesema, mamia ya watu wanatarajiwa kushiriki kwenye matembezi hayo yaliyopewa jina la "Hatua kwa Usalama" ili kuongeza ufuatiliaji kuhusu hali mbaya ya maisha ya watu waliopoteza makazi kutokana na mapambano na maafa ya kimaumbile barani Afrika.

    Wakenya kutoka hali mbalimbali, wakiwemo watu mashuhuri, maofisa wa serikali na wanadiplomasia wataungana na mamia ya wakimbizi kutoka nchi 13 za Afrika kushiriki kwenye matembezi hayo yanayofanyika kwa mara ya kwanza.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako