• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kongamano la pili la matangazo ya kimataifa kuhusu "Njia ya hariri baharini ya karne ya 21" lafunguliwa China

    (GMT+08:00) 2018-09-20 09:48:11

    Kongamano la pili la matangazo ya kimataifa kuhusu "Njia ya hariri baharini ya karne ya 21" lilifunguliwa jana mjini Zhuhai, China.

    Kwenye kongamano hilo linaloandaliwa na Kituo kikuu cha Radio na Televisheni cha China na serikali ya mkoa wa Guangdong, naibu mkuu wa idara ya uenezi ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China ambaye pia ni mkuu wa Kituo Kikuu cha Radio na Televisheni cha China Bw. Shen Haixiong amesema, huu ni mwaka wa 40 tangu China ianze kutekeleza sera ya mageuzi na ufunguaji mlango, na pia ni mwaka wa tano tangu rais Xi Jinping wa China atangaze pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja". Kongamano hilo litaonesha utekelezaji wa miradi mipya katika "Njia ya hariri baharini ya karne ya 21", na kupeana matunda mapya katika mawasiliano kati ya tamaduni tofauti. Amesema Kituo kikuu cha radio na televisheni cha China kitabeba jukumu lake kutoa sauti ya China kwa hatua madhubuti, kulinda kithabiti utaratibu wa biashara ya pande nyingi, na kueneza nadharia ya jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako