• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri mkuu wa China asisitiza umuhimu wa utaratibu wa biashara ya pande nyingi

    (GMT+08:00) 2018-09-20 19:05:21

    Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang amesisitiza umuhimu wa kulinda utaratibu wa kimataifa wa biashara wa pande nyingi.

    Bw. Li ameyasema hayo leo mjini Tianjin alipokutana na wajumbe wa viwanda, mambo ya fedha, jopo la mabingwa na vyombo vya habari waliohudhuria mkutano wa Baraza la Davos. Amesema utaratibu wa kimataifa wa biashara wa pande nyingi ulifikiwa baada ya mazungumzo kati ya nchi nyingi duniani, na umetekelezwa kwa miaka mingi. Hivi sasa ingawa baadhi ya nchi zinafanya majadiliano ya biashara huria ya pande mbili, lakini utaratibu wa kimsingi wa biashara ya pande nyingi unapaswa kulindwa.

    Bw. Li amesema wakati wa kuendeleza biashara huria duniani, kuna mivutano ya aina mbalimbali, lakini inaweza kutatuliwa kwa mazungumzo, na kugeuza utaratibu wa kimataifa wa biashara wa pande nyingi, ili kuufanya kuendana na mahitaji ya maendeleo shirikishi ya dunia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako