• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda:Uganda kuwekeza kwenye kawi ya nuklia

    (GMT+08:00) 2018-09-20 19:50:20
    Waziri wa masuala ya ndani ya nchi nchini Uganda Simon D Ujanga amesema Uganda inajiandaa kuwekeza katika kawi ya nuklia ili kuimarisha sekta ya viwanda.

    Amesema wana imani kwamba kawi hiyo itapunguza mahitaji ya umeme nchini humo.

    Nchi hiyo sasa inataka kushirikiana na Austria kuanzisha miradi hiyo itakayochangia maendeleo ya uchumi pamoja na kuimarisha usalama.

    Nchi hizi mbili zitahakikisha mradi huu unakamilika kwa mda ufaao.

    Huku hayo yakijiri,wizara ya kilimo na uvuvi inataka kuanzisha bima ya kilimo itakayowakinga wakulima dhidi ya hali mbaya ya hewa kuanzia mwaka ujao.

    Wakulima aidha watapewa mikopo chini ya mradi huo .

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako