• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • UNEP yasema sekta ya uchukuzi ni chanzo kikuu cha uchafuzi wa hewa barani Afrika

    (GMT+08:00) 2018-09-21 09:49:21

    Mkurugenzi wa kanda ya Afrika wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa UNEP Bibi Juliette Koudenoukpo amesema, sekta ya uchukuzi ni chanzo kikuu kinachochangia uchafuzi wa hewa barani Afrika.

    Amesema, hali hiyo inatokana na ufanisi mdogo wa matumizi ya nishati wa magari yaliyotumiwa, upungufu wa sera na kanuni za kuagiza magari kutoka nje na uwezo mdogo wa manunuzi ya watu barani humo.

    Bibi Koudenoukpo amesema hayo katika kongamano kuhusu mabadiliko ya usafiri barani Afrika kupitia utatuzi wenye uvumbuzi lililofanyika jijini Nairobi, huku akiongeza kuwa nchi za Afrika zinatakiwa kuweka vigezo vya sifa ya hewa ili kusaidia kutunga sera.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako