• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Polisi wa Ethiopia wakamata maofisa wa serikali kwa kushindwa kutekeleza majukumu yao wakati wa vurugu

    (GMT+08:00) 2018-09-21 10:14:35

    Serikali ya jimbo la Oromia la Ethiopia imetangaza kuwakamata maofisa wa usalama wa jimbo hilo na maofisa wa serikali kutokana na kushindwa kutekeleza majukumu yao wakati wa vurugu zilizotokea hivi karibuni katika kitongoji cha mji mkuu wa nchi hiyo Addis Ababa.

    Habari zinasema mkuu wa ofisi ya mawasiliano wa jimbo hilo Bw. Lencho amesema idadi ya vifo vya watu kwenye vurugu zilizotokea hivi karibuni huko Burayu na eneo jirani imefikia 26, na watatu walifia hospitali.

    Bw. Lencho hakutaja majina ya maofisa hao, na kusema amani imerejeshwa katika maeneo yaliyoathirika.

    Matukio ya hivi karibuni yalitokea baada ya mapigano kati ya wenyeji wa huko na vijana kutoka maeneo ya jirani ambao walikwenda kusherehekea kurudi kwa kiongozi wa kundi la waasi kutoka uhamishoni.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako