• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu 94 wafariki katika ajali ya kivuko nchini Tanzania

    (GMT+08:00) 2018-09-21 17:11:24

    Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Tanzania Bw. John Mongella amesema, mpaka sasa, idadi ya watu waliofariki kwenye ajali ya kuzama kwa kivuko cha MV Nyerere kilichokuwa kikitokea Mwanza imefikia 94 huku wengine 37 wakiokolewa.

    Habari zinasema, kivuko hicho chenye uwezo wa kubeba abiria 100, kilikuwa na abiria zaidi ya 100 wakati ajali hiyo inatokea.

    Bw. Mongella amesema, zoezi la uokoaji bado linaendelea.

    Kivuko hicho kilizama kwenye Ziwa Victoria saa mbili baada ya kuanza safari yake.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako