• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yajitahidi kuboresha mazingira kwa ajili ya makampuni nchini humo

    (GMT+08:00) 2018-09-21 17:24:17

    Kongamano la mwaka 2018 la masuala muhimu ya kitaifa limefanyika jana hapa Beijing. Wajumbe waliohudhuria kongamano huo wanaona hivi sasa China inajitahidi kuboresha mazingira ya biashara, ili kuyahamasisha zaidi makampuni.

    Mwaka huu namna ya kuboresha mazingira ya biashara, kupunguza mzigo wa makampuni madogo na yenye ukubwa wa kati, na kuhimiza maendeleo ya sekta za uzalishaji ni masuala muhimu yanayofuatiliwa zaidi na mikutano ya baraza la serikali la China. Kwenye mkutano uliofanyika jana, mwenyekiti wa bodi ya kampuni ya Hengtong Bw. Cui Shangliang anaona makampuni binafsi zimekuwa ni nguvu muhimu ya kuhimiza maendeleo ya uchumi na utulivu wa jamii nchini China, huku serikali ikitoa sera za aina mbalimbali za kuunga mkono makampuni hayo. Bw. Cui anasema,

    "Tangu mkutano mkuu wa 18 wa Chama cha Kikomunisti cha China ulipofanyika, serikali imepunguza uingiliaji na vizuizi ili kustawisha soko. Haswa baada ya mkutano mkuu wa 19 wa Chama cha Kikomunisti cha China, serikali imetangaza mageuzi, na kupunguza kodi wa makampuni kwa kiasi kikubwa. Kampuni yetu ya Hengtong imehesabu kwa ujumla, na kutambua kuwa, kodi yetu kwa mwaka huu itapungua kwa yuan kati ya milioni 400 na 500. Hii ni faida halisi kwetu."

    Katika miaka ya hivi karibuni, China imeshikilia kuhimiza mageuzi kuhusu makampuni, ambayo yameinua kiwango cha ufunguaji mlango cha uchumi, kuhamasisha ustawi wa soko na uvumbuzi wa jamii, na kuongeza ufanisi na sifa ya huduma za serikali. Wakati huo huo, jumuiya ya kimataifa ina matakwa mapya kwa China kupunguza vizuizi vya soko na kuongeza nguvu ya kulinda haki miliki za ujuzi. Mkurugenzi wa idara ya sheria ya Kamati Kuu ya Maendeleo na Mageuzi ya China Bibi Yang Jie amesema, kuanzisha mazingira bora ya biashara ni agizo jipya la baraza la serikali la China, ambalo limeunda kikundi maalumu cha waratibu mahususi kushughulikia kazi hii. China itaharakisha kufanya mambo matatu. Anasema,

    "Kwanza ni kuharakisha mfumo wa kulinda haki miliki za ujuzi unaolingana na vigezo vya kimataifa. Pili ni kuharakisha mchakato wa mageuzi ya mafungamano ya forodha. Na tatu ni kuharakisha kuyapa makampuni yenye uwekezaji kutoka nje haki sawa na makampuni ya ndani."

    Ili kupunguza vizuzi na kustawisha soko, katika miaka ya hivi karibuni China imesukuma mbele mageuzi ya mifumo ya mambo ya biashara. Naibu mkurugenzi wa ofisi ya uandikishaji ya idara kuu ya usimamizi wa soko ya China Bibi Chen Ye amesema idara hiyo itahimiza makampuni kupata uhuru zaidi katika biashara zao kutokana na mageuzi ya mifumo ya mambo ya biashara. Anasema,

    "Mwaka huu, baraza la serikali limepanga hatua muhimu mbili. Kwanza ni kuboresha utaratibu wa kuidhinisha uandikishaji wa makampuni, na pili ni kupunguza muda wa kuanzisha makampuni kuwa ndani ya siku 8.5."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako