Shirika la Habari la Iran limeripoti kuwa takribani watu 24 wameuawa kutokana na shambulio la kigaidi lililotekelezwa jana wakati wa gwaride la kijeshi katika mji wa Ahvaz nchini humo.
Miongoni mwa waliouwawa ni wanajeshi na raia waliokusanyika kutazama gwaride hilo la kijeshi, ambapo zaidi ya watu 50 walijeruhiwa.
Inaelezwa kuwa leo asubuhi, watu wenye silaha wakiwa wamevalia sare za kikundi cha wapiganaji cha IGRC kilishambulia gwaride ambalo lilikuwa maalum kuadhimisha kumbukumbu ya vita vya Iraq na Iran.
Aidha wapiganaji wawili waliuwawa huku wengine wawili wakishikiliwa.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |