• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • UAE yakanusha shutuma za Iran kuhusu shambulizi la kigaidi

    (GMT+08:00) 2018-09-24 09:20:02

    Waziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Falme za Kiarabu UAE Bw. Anwar Gargash amekanusha shutuma zilizotolewa na Iran kuwa washirika wa Marekani wa nchi za ghuba wanahusika na shambulizi lililotokea nchini Iran.

    Wanaume wanne wenye silaha asubuhi ya Jumamosi walishambulia gwaride la kuadhimisha vita kati ya Iran na Iraq iliyoanzia mwaka 1980 hadi 1988 mjini Ahvaz, kusini magharibi mwa Iran, na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 29 wakiwemo wanamgambo wawili. Waziri wa mambo ya nje wa Iran Bw. Javad Zarif amesema Marekani na washirika wake wanahusika na shambulizi hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako