• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Gofu, Tiger Woods ashinda taji la Ubingwa baada ya miaka 5 kupita

    (GMT+08:00) 2018-09-24 10:31:49

    Kwa kile kinachodhaniwa kuwa ni kuzaliwa upya kwa uwezo wa bingwa wa kihistoria wa mchezo wa gofu duniani Tiger Woods wa Marekani, nyota huyo jana ameshinda ubingwa wa mashindano ya kimataifa ya Atlanta kwa alama za juu kabisa.

    Woods ambaye ana rekodi ya ubingwa mara 14 wa michuano mikubwa ya gofu, alifanikiwa kushinda jana ikiwa ni baada ya miaka mitano kupita tangu akumbwe na misukosuko iliyopelekea kipaji chake kushuka na kukosa mvuto.

    Aidha hili pia ni tumaini kubwa kwa taifa la Marekani kuelekea michuano ya kimataifa ambapo pia Woods ameteuliwa miongoni mwa wachezaji.

    Nafasi ya pili kwenye mashindano ya Atlanta ilikwenda kwa Roy Mcllroy wa Ireland Kaskazini na nafasi ya tatu ikienda kwa Justin Rose kutoka Uingereza.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako