• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri wa nishati wa Saudi Arabia asema OPEC haitaongeza uzalishaji wa mafuta

    (GMT+08:00) 2018-09-24 18:41:21

    Waziri wa nishati wa Saudi Arabia Bw. Khalid al-Falih amesema, nchi zinazozalisha mafuta hazijafikia makubaliano juu ya kuongeza uzalishaji wa mafuta.

    Bw. Al Falih amesema hayo wakati wa Mkutano wa kumi wa ngazi ya mawaziri wa Jumuiya ya Nchi zinazozalisha Mafuta (OPEC) na nchi zinazozalisha mafuta zisizo wanachama wa jumuiya hiyo uliofanyika mjini Algiers, Algeria. Amesema, hivi sasa nchi zinazozalisha mafuta zinafikiria kudumisha utulivu wa bei ya mafuta ya kimataifa katika kiwango cha dola 80 za kimarekani kwa pipa ili kunanufaisha nchi zinazozalisha mafuta na nchi zinazotumia mafuta.

    Pia amesema utoaji wa mafuta katika soko la kimataifa unaweza kuhakikishwa kupitia hatua mwafaka.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako