• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waraka wa China waonesha ukweli wa migogoro ya kiuchumi na kibiashara kati yake na Marekani

    (GMT+08:00) 2018-09-24 19:22:18

    China imetoa waraka unaoeleza undani wa migogoro ya kiuchumi na kibiashara kati yake na Marekani pamoja na msimamo wa China. Waraka huo umefafanua kuwa ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara ni wa kunufaishana, na kukanusha lawama ya Marekani iliyowekwa kwenye ripoti ya uchunguzi wa kipengele cha 301 cha sheria ya biashara ya Marekani dhidi ya China…….

    Waraka huo unaisaidia jumuiya ya kimataifa kutambua kihalisi chanzo cha migogoro hiyo na kuelewa mapendekezo yaliyotolewa na China katika kuongeza uaminifu kati yake na Marekani, kuhimiza ushirikiano, kusimamia na kudhibiti migogoro hiyo.

    Kwanza waraka huo umeeleza kuwa kanuni ya kunufaishana na kusaidiana ya Shirika la Biashara Duniani (WTO) inazingatia kipindi tofauti nchi mbali mbali zilizokuwa, ambayo imeonesha usawa halisi wa kimataifa. Kanuni zinazoshikiliwa na Marekani za "biashara yenye usawa" na "ufunguaji mlango kwa kunufaishana" zinakataa kukubali kuwepo kwa hali tofauti kati ya nchi mbalimbali na kutozingatia haki ya kujiendeleza kwa nchi zinazoendelea, zitaathiri uchumi na viwanda za nchi zinazoendelea na kusababisha kutokuwa na usawa kwenye maeneo makubwa zaidi.

    Pili waraka huo umefafanua msimamo wa China kuhusu suala hilo, kwamba China inalinda kithabiti heshima ya taifa na maslahi yake muhimu, kusukuma mbele kwa hatua madhubuti maendeleo chanya ya uhusiano wa kiuchumi na kibiashara kati yake na Marekani, na kulinda kithabiti na kuhimiza mageuzi ili kukamilisha utaratibu wa biashara ya pande nyingi. Pia China inalinda kithabiti hakimiliki ya ujuzi, maslahi ya wafanyabiashara nchini humo, kukuza mageuzi na ufunguaji mlango, kuhimiza ushirikiano wa kunufaishana na nchi nyingine zilizoendelea na zile zinazoendelea na kuhimiza ujenzi wa jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja.

    Tatu waraka huo umetangaza njia ya kutatua mikwaruzano hiyo, ukisema China inapenda kufanya juhudi katika kujenga utaratibu mpya wa kiuchumi na kibiashara ulio na uwiano, kuvumiliana na kupata maendeleo kwa pamoja. Pia umesisitiza kuwa China iko wazi katika kufanya mazungumzo lakini lazima yafanyike kwa msingi wa kuheshimiana, kutendeana kwa usawa na kutoa ahadi zitakazotimizwa, badala ya kufanyika chini ya sharti la kutozwa ushuru na kuleta hasara kwa haki ya kujiendeleza. Pia waraka huo umesisitiza kuwa hakutakuwa na mshindi katika vita vya kibiashara, na utatuzi wa mikwaruzano ya kiuchumi na kibiashara kati ya China na Marekani inatakiwa kurejea katika njia sahihi kwa kuzingatia maslahi ya wananchi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako