• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kampuni ya China yajenga handaki kubwa zaidi la reli katika eneo la Afrika Mashariki

  (GMT+08:00) 2018-09-25 08:44:17

  Kampuni ya ujenzi wa reli na madaraja ya China inayojenga awamu ya pili ya mradi wa reli ya SGR nchini Kenya, imechimba handaki kubwa zaidi la reli katika eneo la Afrika Mashariki. Handaki hilo la Ngong lenye urefu wa kilometa 4.5, ni sehemu muhimu zaidi ya awamu ya pili ya mradi wa reli ya SGR nchini Kenya.

  Meneja mkuu wa mradi wa reli ya SGR Bw. An Aijun amesema njia ya handaki inapunguza gharama na ina ufanisi kwenye kuendana na mazingira tofauti ya kujiografia na hali ya maji chini ya ardhini.

  Bw. An amesema watahakikisha kuwa ubora na usalama vinahakikishwa, kwenye mchakato wote wa ujenzi na usimamizi wa mradi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako