• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Katibu mkuu wa UN asema kati ya dola trilioni 5 na trilioni  7 zinahitajika kila mwaka kutekeleza malengo ya maendeleo ya milenia

  (GMT+08:00) 2018-09-25 08:44:45

  Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres amesema kati ya dola za kimarekani trilioni 5 na trilioni 7 zinahitaji kuwekezwa kila mwaka ili kutimiza malengo ya maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa ya mwaka 2030.

  Akiongea kwenye mkutano wa ngazi ya juu kuhusu ukusanyaji wa fedha kwa ajili ya malengo ya maendeleo endelevu, katibu mkuu amesema ili kutimiza malengo hayo kuna haja ya kuongeza ukusanyaji wa fedha na uwekezaji. Hata hivyo Bw. Guterres amesema hiyo haitakuwa kazi rahisi kwa kuwa mahitaji hayo ya fedha ni makubwa sana.

  Bw. Guterres amesema mafanikio kiasi yamepatikana kwenye ukusanyaji wa fedha, lakini juhudi zaidi zinatakiwa kufanywa. Pia amezikumbusha nchi zote zilizoendelea kutimiza ahadi walizotoa kwenye ajenda ya utekelezaji ya Addis Ababa, na kuzisaidia nchi zinazoendelea kuwa na mazingira ya kukusanya fedha za ndani, ikiwa ni pamoja na mageuzi ya kodi na utawala bora.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako