• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Soka, Tuzo za FIFA 2018: Luka Modric mchezaji bora wa dunia, Marta wa Brazil bora upande wa wanawake

  (GMT+08:00) 2018-09-25 08:55:56

  Luca Modric ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa dunia wa FIFA kwa mwaka 2018, akiwashinda Cristiano Ronaldo wa Ureno na Mohamed Salah wa Misri.

  Katika tuzo hizo zilizotolewa mjini London, Marta wa Brazil ameibuka kidedea kwa upande wa wanawake akiwashinda Dzsenifer Marozsan wa Ujerumani na Ada Hegerberg wa Norway.

  Tuzo ya golikipa bora ilikwenda kwa Thibout Cortiuos wa Ubelgiji, na tuzo ya goli bora la mwaka ikitwaliwa na Mohamed Salah wa Misri.

  Kocha bora wa timu ya wanaume aliibuka Didier Deschamps wa Ufaransa, na kwa upande wa wanawake alikuwa Reynald Pedros wa Ufaransa pia.

  Aidha, FIFA ilitaja kikosi bora cha mwaka 2018 ambacho, golikipa ni David DeGea wa Manchester United, walinzi ni Dan Alves wa PSG, Rafael Varane, Sergio Ramos na Marcelo wote kutoka Real Madrid.

  Viungo ni Luka Modric wa Real Madrid, N'Golo Kante na Eden Hazard wote kutoka Chelsea, na upande wa Ushambuliaji ni Kylian Mbappe wa PSG, Lionel Messi wa Barcelona na Cristiano Ronaldo wa Juventus.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako