• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Maofisa wa China wasema athari zinazotokana na mikwaruzano ya kiuchumi na kibiashara kati yake na Marekani zinadhibitika

    (GMT+08:00) 2018-09-25 18:03:50

    Maofisa wa Wizara ya biashara ya China, Kamati ya maendeleo na mageuzi ya taifa, Wizara ya viwanda na habari, Wizara ya fedha, na Idara ya hakimiliki ya ujuzi ya taifa wamejumuika kwenye Ofisi ya habari ya Baraza la serikali la China, kujibu maswali kuhusu mikwaruzano ya kiuchumi na kibiashara kati ya China na Marekani yanayofuatiliwa zaidi. Kitendo cha Marekani cha kuchochea mikwaruzano ya kiuchumi na kibiashara kati yake na China kimefuatiliwa sana na dunia nzima katika mwaka huu. Serikali ya China imetangaza waraka unaofafanua ukweli wa mikwaruzano hiyo na msimamo wa China, hatua ambayo inalenga kuonesha hali halisi ya uhusiano wa kiuchumi na kibiashara kati yake na Marekani, na msimamo wa China ili kutafuta ufumbuzi mwafaka wa suala hilo. Naibu waziri wa biashara wa China ambaye pia ni naibu mwakilishi wa mazungumzo ya biashara ya kimataifa Bw. Wang Shouwen amesisitiza kuwa, China iko wazi katika kutatua mikwaruzano hiyo kwa njia ya mazungumzo, na lini mazungumzo hayo yatarejeshwa itategemea na nia ya Marekani. Bw. Wang anasema:

    "Matokeo ya mazungumzo hayo yatapatikana kwa kufuata msingi wa kutendeana kwa usawa na kuheshimiana. Hivi sasa vikwazo vikubwa vinavyowekwa na Marekani ni kama kuweka kisu shingoni mwa mtu, ambayo si mazungumzo yenye usawa. Aidha ni lazima mazungumzo hayo yafanyike kwa moyo wa dhati, na kufuata ahadi zilizotolewa. Hadi sasa duru nne za mazungumzo ya ngazi ya juu kati ya China na Marekani zimefanyika na kupata maafikiano mengi, lakini upande wa Marekani umepuuza makubaliano hayo na kuendelea vitendo vya vizuizi, hatua ambayo imekwamisha mazungumzo kati ya pande hizo mbili."

    Akizungumzia hatua ya Marekani ya kutoza ushuru kwa bidhaa zenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 200 zinazoagizwa kutoka China, naibu mkurugenzi wa Kamati ya maendeleo na mageuzi ya China Bw. Lian Weiliang amesema hatua hiyo itaathiri kiasi uchumi wa China, lakini kwa ujumla matishio yanayotokana na hatua hiyo yanadhibitika, na China ina uwezo wa kukabiliana na athari hizo kwa kupanua mahitaji ya ndani. Bw. Lian anasema:

    "Mwaka 2017 thamani ya jumla ya uchumi ilikuwa imefikia dola za kimarekani trilioni 12.7, huku thamani ya uuzaji wa bidhaa nje ikifikia dola za kimarekani trilioni 2.26, na dola za kimarekani bilioni 200 ambayo inachukua asilimia 8.8 katika thamani ya jumla ya uuzaji wa bidhaa nje. Kwa upande mwingine, China ina idadi ya watu bilioni 1.4, kiasi ambacho kinazidi idadi ya jumla ya makundi ya kiuchumi yaliyoendelea, na wastani wa mapato ya wananchi yanakaribia dola za kimarekani bilioni 900, hali ambayo imeonesha kuwa soko la ndani nchini China lina mustakabali mzuri."

    Naibu waziri wa viwanda na habari wa China Bw. Luo Wen ameeleza kuwa, kitendo cha Marekani cha kujipendelea upande mmoja na kujilinda kibiashara kimezilazimisha nchi mbalimbali duniani kuchukua hatua za majibizano. Kutokana na hali hiyo, utaratibu wa uchumi na biashara wa kimataifa unaweza kuharibiwa au hata kupinduliwa, huku tishio la kutokuwa na utaratibu linaloikabili minyororo ya viwanda duniani likizidi kuongezeka.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako