• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Tawa yatakiwa kuongeza makusanyo hadi Sh100 bilioni ifikapo 2020.

    (GMT+08:00) 2018-09-25 19:01:33

    Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori nchini Tanzania (Tawa), imetakiwa kuongeza makusanyo yake kutoka Sh47 bilioni kwa mwaka hadi Sh100 bilioni ifikapo mwaka 2020.

    Mwenyekiti bodi ya Tawa, Meja Jenerali mstaafu, Hamis Semfuko alitoa maagizo hayo jana Septemba 22, 2018 wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya maagizo ya bodi hiyo ambayo inamaliza muda wake.

    Alisema lengo hilo linawezekana kwani Tawa tangu ilipoanza kazi rasmi mwaka 2006 imeweza kuwa na mafanikio makubwa baada ya kuanza fedha kidogo kiasi cha Sh 350 milioni pekee.

    Mwenyekiti huyo pia aliwataka wafanyakazi wa mamlaka hiyo kuendelea kubadilika katika utendaji kazi wao, wawe wazalendo, waadilifu na kupiga vita rushwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako