• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Russia yasema kutoa mfumo wa ulinzi wa anga wa makombora wa aina ya S-300 kwa Syria haulengi upande wa tatu

    (GMT+08:00) 2018-09-26 08:37:32

    Katibu wa habari wa rais Vladmir Putin wa Russia Bw. Dmitry Peskov amesema, kutoa mfumo wa ulinzi wa anga wa makombora wa aina ya S-300 kwa Syria hakulengi upande wa tatu, lakini ni kwa ajili ya kulinda usalama wa wanajeshi wa Russia nchini humo tu.

    Mkurugenzi wa idara ya kupunguza na kuzuia kuenea kwa silaha ya wizara ya mambo ya nje ya Russia Bw. Victor Fedolovich Yermakov amesema, kitendo hicho cha Russia kitatuliza hali ya kikanda, kwani kama inahitajika, mfumo huo unaweza kufunga baadhi ya maeneo ya anga na kulinda usalama wa wanajeshi wa Russia wanaotekeleza majukumu yao ya kimataifa.

    Bw. Yermakov amesisitiza kuwa, mfumo huo ni wa kujilinda tu. Kutoa misaada ya kijeshi kwa wenzi ni haki ya kila nchi, na Russia haitaacha kitendo hicho kama Marekani inavyotarajia.

    Habari zinasema, waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema, jeshi la ulinzi la Israel (IDF) litaendelea kushambulia maeneo yaliyolengwa ya Iran nchini Syria.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako