• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bw. Guterres asema ushiriki wa pande nyingi upo hatarini wakati unapohitajika zaidi

    (GMT+08:00) 2018-09-26 09:20:19

    Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameonya kuwa ushiriki wa pande nyingi upo hatarini wakati ambao unahitajika zaidi duniani.

    Akiongea na viongozi mbalimbali duniani waliohudhuria mjadala wa ngazi ya juu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Bw. Guterres ameeleza kuwa hivi sasa kuna tatizo kubwa la kutoaminiana katika taasisi za kitaifa, baina ya nchi na hata kwenye sheria za kimataifa. Amesisitiza kuwa ndani ya nchi, watu wanapoteza imani na mifumo ya kisiasa, matabaka yanaongezeka na upinzani dhidi ya utawala unazidi. Aidha amesema ushirikiano miongoni mwa nchi umekuwa hauna uhakika na mgumu zaidi, na mgawanyiko kwenye Baraza la Usalama nao pia umeongezeka.

    Bw Guterres ameongeza kuwa wameweka msingi wa ushirikiano wa kimataifa kwa miongo mingi, pamoja na kuanzisha taasisi, kanuni na sheria ili kuongeza maslahi ya nchi mbalimbali. Hivyo vitu vyote hivyo havipaswi kutumiwa vibaya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako