• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Afisa wa Burundi asema ni vigumu kufikia lengo la kuwarudisha wakimbizi elfu 72 wa Burundi

  (GMT+08:00) 2018-09-26 09:38:27

  Msaidizi wa waziri wa mambo ya ndani wa Burundi Bw. Therence Ntahiraja amesema itakuwa vigumu kufikia lengo la kuwarudisha nyumbani wakimbizi elfu 72 wa Burundi kutoka Tanzania kabla ya mwezi Desemba mwaka huu kama ilivyofikiwa kwenye mkutano wa kurejesha wakimbizi kwa hiari mwezi Machi.

  Hadi mwishoni mwa mwezi huu, ni wakimbizi 37,800 tu wa Burundi waliorejeshwa nyumbani, na itakuwa ngumu kufikia lengo hilo. Shirika la UNHCR limeshindwa kurejesha wakimbizi 2,000 kwa wiki kwa sababu ya kutokuwa na vifaa vya kutosha.

  Kulingana na takwimu za UNHCR, kuna wakimbizi laki 383,283 wa Burundi ambao hawajarejea nyumbani, na zaidi ya nusu wanaishi Tanzania.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako