Timu ya taifa ya Rwanda, leo inaanza kampeni zake za kuwania ubingwa wa mashindano ya Baiskeli ya kimataifa ya Cameroun, ikiwa ni baada ya timu hiyo kukosekana tangu mashindano ya mwaka 2016.
Kocha mkuu wa timu hiyo, Felix Sempoma amesema kutokana na maandalizi waliyoyafanya ni wazi kuwa watafanikiwa kushinda mbio hizo.
Timu ya Rwanda katika mashindano hayo inaundwa na Jean Bosco Nsengimana, Bonaventure Uwizeyimana, Janvier Rugamba, Eric Manizabayo na Michel Uwiduhaye.
Katika siku ya kwanza leo, washiriki watachuana umbali wa kilomita 92 ndani ya mji wa Douala.
| © China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |