• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • TADB na NIRC wasaini makubaliano ya kuboresha vyanzo vya umwagiliaji Tanzania

    (GMT+08:00) 2018-09-26 18:37:27

    Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) na Tume ya Taifa ya Umwagiliaji (NIRC),wamesaini makubaliano yatakayowezesha kuboresha vyanzo na miundombinu ya umwagiliaji nchini humo.

    Akizungumza wakati wa utiliaji saini wa makubaliano hayo jijini Dar es Salaam jana,Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB,Japhet Justine,alisema makubaliano hayo yanalenga kuiwezesha Tume ya umwagiliaji kuendeleza vyanzo vya maji ili viwasaidie wakulima na kuimarisha sekta ya kilimo kwa ujumla.

    Justine alisema mpaka sasa wameshawezesha miradi tisa ya umwagiliaji na mingine minne ambayo bado ipo kwenye uchambuzi kabla ya kufadhiliwa ,na kuongeza kuwa miundombinu ya umwagiliaji ni muhimu katika kilimo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako