• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yafanya juhudi katika kujenga vyombo vya habari vyenye uwezo mkubwa wa kuelekeza, kutangaza na wa kushawishi

    (GMT+08:00) 2018-09-26 21:08:17

    Huu ni mwaka wa miaka 60 tangu kuzinduliwa kwa kituo cha televisheni cha taifa la China CCTV na kuanzishwa kwa matangazo ya televisheni nchini humo.

    Rais Xi Jinping ametoa barua ya pongezi akisifu mafanikio makubwa katika matangazo ya televisheni, na maendeleo yaliyopatikana baada ya kuundwa kwa Kituo Kikuu cha Radio na Televisheni cha Taifa cha China. Pia ametoa maagizo katika kuhimiza kituo hicho na kazi ya vyombo vya habari ya Chama cha Kikomunisti cha China CPC kupata maendeleo mapya wakati wa hali mpya ya sasa. Barua hiyo ya rais Xi ni msukumo mkubwa kwa Kituo Kikuu cha Radio na Televisheni cha China pamoja na wafanyakazi wa matangazo ya televisheni kote nchini. Ni lazima tujifunze kwa makini na kutekeleza vizuri maagizo yaliyowekwa kwenye barua hiyo ili kuweka mustakabali mpya wa mambo ya televisheni nchini China.

    Kwenye barua yake, rais Xi amesema matangazo hayo ni sehemu muhimu ya kazi za vyombo vya habari vya CPC. Katika miaka 60 iliyopita, kituo cha CCTV kikiwa nguzo muhimu katika mambo ya televisheni ya taifa, daima kilishikilia upande sahihi na kubeba majukumu yake kikiwa chombo cha habari cha chama, kufanya mageuzi na uvumbuzi, na kupata mafanikio mazuri katika mambo ya televisheni na ya habari nchini China. Mafanikio hayo ni fahari kubwa kwa wafanyakazi wote wa matangazo ya televisheni.

    Hivi sasa China iko kwenye mwanzo mpya wa historia, na itashikamana vizuri kwa kufuata Kamati Kuu ya CPC inayoongozwa na rais Xi Jinping, kushikilia nadharia ya rais Xi kuhusu ujamaa wenye umaalumu wa China, kubeba majukumu yanayostahiki, kupiga hatua katika kujenga vyombo vya habari vyenye kiwango cha juu ambavyo vina uwezo mkubwa wa kuongoza, kupaza sauti na wa ushawishi duniani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako