Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres ametoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kufanya juhudi za pamoja kuanzisha tena mazungumzo ya dhati ili kuondoa kabisa silaha za nyuklia na kutimiza ahadi za kupunguza silaha za nyuklia.
Bw. Guterres amesema hayo kwenye mkutano wa ngazi ya juu wa Baraza Kuu la 73 la Umoja wa Mataifa, ikiwa ni maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya kuondoa silaha za nyuklia. Ameongeza kwamba silaha za nyuklia zinatishia usalama wa dunia na binadamu wote, na kutoa wito kwa nchi mbili kubwa zenye silaha za nyuklia Marekani na Russia kuanzisha tena mazungumzo ya kupunguza silaha la nyuklia.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |