• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Ujerumani wenyeji wa EURO 2024, Uturuki chali EUFA

  (GMT+08:00) 2018-09-28 08:55:53

  Ujerumani imeshinda haki ya kuandaa fainali za kombe la mataifa ya Ulaya, Euro 2024, ikiwazidi Uturuki katika kura zilizopigwa na kamati kuu ya shirikisho la soka ulaya (UEFA) mjini Nyon, Uswisi.

  Washindi mara tatu wa mashindano hayo, Ujerumani walikuwa wenyeji wa fainali za mwaka 1988 na pia wamewahi kuandaa fainali za kombe la dunia katika miaka ya 1974 na 2006.

  Pia watakuwa wenyeji wa michuano ya Olimpiki katika Jiji la Berlin itakayoshirikisha timu 24, na jumla ya michezo 51 kwa siku 32 kati ya Juni na Julai.

  Miji mingine itakayotumika kwa michezo hiyo ni Cologne, Dortmund, Dusseldorf, Frankfurt, Gelsenkirchen, Hamburg, Leipzig, Munich na Stuttgart.

  Rais wa shirikisho la soka la Ujerumani, Reinhard Grindel na Makamu wa Mwenyekiti wa Shirikisho la Soka Uturuki, Servet Yardimci hawakuruhusiwa kupiga kura na wa Denmark pia, Lars-Christer Olsson, uamuzi huo ulichukuliwa kwa kura za Wajumbe wengine 17 wa Kamati Kuu ya UEFA.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako