• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Japan kufanya mapinduzi makubwa Olympic 2020

    (GMT+08:00) 2018-09-28 08:56:22

    Japan ni mwenyeji wa mashindano ya Olympic ya mwaka 2020 inapanga kuyafanya mashindano hayo kuwa ya kwanza katika historia yatakayotawaliwa na teknolojia kwa asilima kubwa kwa kutambulisha mifumo mbalimbali ya kiuendeshaji.

    Nchi hiyo inapanga kutambulisha teknolojia mbalimbali katika mashindano hayo ikiwemo ya kusambaza umeme utakaotumika katika viwanja na matukio ya mashindano kutoka katika vyanzo rafiki na mazingira, maarufu kama 'renewable energy sources' ili kupunguza hewa chafu.

    Pia nchi hiyo inapanga kutengeneza medali za washindi kwenye mashindano hayo zaidi ya 5,000 kutoka katika vyuma chakavu vya simu pamoja na kamera zilizotumika

    Japan pia imeshatambulisha huduma ya usafiri wa taxi usio na dereva pamoja na teknolojia ya kutafsiri lugha mbalimbali kwa kutumia roboti kwaajili ya kupunguza changamoto ya usafiri na lugha kwa watalii watakaohudhuria michuano hiyo.

    Maandalizi hayo yanaendelea huku mabadiliko mengi ya kiteknolojia yakitarajiwa kukamilika ifikapo mwaka 2020 kabla ya uzinduzi rasmi wa mashindano hayo yanayotarajiwa kuanzia 24, Julai hadi 9, Agosti mwaka 2020.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako