• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • VAR kutumika klabu bingwa Ulaya

    (GMT+08:00) 2018-09-28 08:56:47

    Shirikisho la soka barani Ulaya UEFA limetangaza kuwa teknolojia ya usaidizi wa waamuzi 'VAR' itatumika katika mashindano makubwa ya shirikisho hilo yakiwemo ya klabu bingwa Ulaya kuanzia msimu ujao. 2019/20

    Teknolojia hiyo ambayo ilitumika kwa kiasi kikubwa katika michuano ya kombe la dunia mwaka huu nchini urusi, ilionekana kukubalika miongoni mwa wadau na wachambuzi wengi wa soka kuwa inaleta faida nyingi katika mchezo huo.

    taarifa hiyo imeongeza kuwa VAR itatumika katika mchezo wa UEFA Super Cup wa mwaka 2019 ambao utachezwa baada ya kupatikana kwa washindi wa michuano ya klabu bingwa Ulaya na 'Europa League' inayoendelea mwaka huu.

    Pia itaanza kutumika katika michuano ya mataifa ya Ulaya itakayofanyika mwaka 2020, michuano ya 'Europa League' ya mwaka 2020/21 na kwenye fainali ya mashindano yaliyoanzishwa mwaka huu ya ligi ya mataifa ya Ulaya mwaka 2021.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako