• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Idadi ya wakimbizi walioandikishwa nchini Uganda yazidi milioni moja

    (GMT+08:00) 2018-09-28 09:10:55

    Msemaji wa ofisi ya Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa nchini Uganda Bw. Duniya Aslam Khan amesema idadi ya wakimibizi walioandikishwa kwa kuchukuliwa alama za vidole nchini Uganda imezidi milioni moja.

    Bw. Khan amesema hadi sasa wakimbizi milioni 1 kati ya wakimbizi milioni 1.4 wameandikishwa nchini Uganda. Njia hiyo ya utambuzi wa alama ya vidole itasaidia serikali kutathimini idadi ya wakimbizi, ili kuhakikisha wanapatiwa misaada wanayoihitaji kwa ufanisi.

    Tangu mwezi Machi mwaka huu, Uganda ilianza kutumia njia ya alama za vidole katika kuhesabu idadi ya wakimbizi, ili kuhakikisha matumizi mazuri ya fedha kwa ajili ya wakimbizi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako