• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Waziri wa mambo ya nje wa China ahudhuria mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa nchi za BRICS

  (GMT+08:00) 2018-09-28 09:46:37

  Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi jana huko New York alihudhuria mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa nchi za BRICS, na kukubaliana na wenzake kuhusu kutekeleza makubaliano yaliyofikiwa kwenye mkutano wa viongozi wa BRICS uliofanyika mjini Jorhannesburg, Afrika Kusini, kuimarisha mawasiliano ya kimkakati, kuzidisha ushirikiano, kuongeza maingiliano kati ya watu na watu, kuleta manufaa kwa pande zote, na kutekeleza ajenda ya mwaka 2030 ya maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa.

  Siku hiyo Bw. Wang Yi pia alihudhuria mkutano kuhusu suala la nyuklia la Peninsula ya Korea, na kusisitiza kuwa pande mbalimbali zinapaswa kufanya juhudi kujenga Peninsula hiyo iwe sehemu yenye amani na utulivu, isiyo na silaha za nyuklia, na yenye ushirikiano wa kunufaishana.

  Amesema, pande mbalimbali zinapaswa kuendelea kutekeleza kikamilifu, kwa pande zote, na kwa usahihi maamuzi husika ya baraza la usalama la Umoja wa Mataifa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako