• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wajumbe wa Afrika wahimiza Sudan Kusini kutekeleza makubaliano ya amani

    (GMT+08:00) 2018-09-28 09:47:09

    Baadhi ya wanadiplomasia wa nchi za Afrika nchini Sudan Kusini wamewataka viongozi wa nchi hiyo kutopoteza fursa ya makubaliano ya amani yaliyosainiwa hivi karibuni, na kuhakikisha wanayatekeleza kikamilifu.

    Shirikisho la wanadiplomasia wa Afrika nchini Sudan Kusini linasema makubaliano ya hivi karibuni yanaleta matumaini ya kurejesha utulivu, na pande mbalimbali zilizosaini makubaliano hayo zinapaswa kusimamisha vita.

    Kiongozi wa shirikisho hilo ambaye pia ni balozi wa Kenya nchini humo, Cleland Leshore amesema Afrika inataka kuona Sudan Kusini yenye amani na ustawi, na ndoto hiyo inatimizwa kama makubaliano ya amani yatatekelezwa kikamilifu.

    Habari nyingine zinasema, mkuu wa jeshi la Sudan Kusini SPLA Jok Riak jana alieleza ahadi ya jeshi hilo kutekeleza makubaliano ya amani yaliyosainiwa nchini Ethiopia. Amesema mauaji ya kikabila yameiathiri sana nchi hiyo katika miaka minne iliyopita, na jeshi la SPLA lina hamu kubwa ya kutafuta amani nchini hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako