• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yapinga Marekani kuiwekea vikwazo bila msingi wowote

    (GMT+08:00) 2018-09-28 10:29:20

    Msemaji wa Wizara ya ulinzi ya China Bw. Ren Guoqiang amesema Marekani inabeba lawama zote kwa matatizo yaliyopo katika uhusiano wa majeshi ya nchi hizo mbili, na inatakiwa kuchukua hatua kwa makini na kwa upevu.

    Bw. Ren ameyasema hayo kwenye mkutano na waandishi wa habari alipojibu maswali kuhusu Marekani kuiuzia silaha Taiwan, vikwazo dhidi ya idara ya kijeshi ya China na uwepo wa ndege za mashambulizi za Marekani katika Bahari ya Kusini ya China.

    Bw. Ren Guoqiang amesisitiza kuwa China inapinga hatua hizo na kuitaka Marekani ichukue hatua za kuboresha na kuendeleza uhusiano kati ya majeshi ya China na Marekani, na kushirikiana na China ili kuufanya uhusiano huo uwe na nguvu ya kutuliza uhusiano kati ya nchi hizo mbili.

    Katika suala la mauzo ya silaha, Bw. Ren amesema suala hilo halihusu idadi, bali maana yake. Mauzo ya silaha yanaharibu vibaya uhusiano wa kijeshi kati ya China na Marekani, na amani na utulivu katika kando mbili za mlango bahari wa Taiwan. Na kuhusu vitendo vya uchokozi katika Bahari ya Kusini ya China, Bw. Ren amesema China itaendelea kuchukua hatua za lazima kushughulikia hali hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako