• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mfumo wa pande nyingi wapambana na hatua ya upande mmoja katika mkutano mkuu wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa

    (GMT+08:00) 2018-09-28 16:54:03

    Wakati mkutano mkuu wa baraza kuu la 73 la Umoja wa Mataifa unafanyika, hatua za upande mmoja na kujilinda kibiashara zinaongezeka na kuharibu mfumo wa kimataifa ambao umoja wa mataifa ni kiini chake, na kumbisha ongezeko dhaifu la maendeleo ya uchumi wa dunia. Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres amesema, sasa ni wakati ambao binadamu wanahitaji zaidi mfumo wa pande nyingi. Hivyo kaulimbiu ya mkutano mkuu huo imekuwa "Kuufanya Umoja wa Mataifa uhusiane na Watu Wot, na kujenga jamii yenye amani, usawa na endelevu kupitia uongozi wa dunia na mgawanyo wa majukumu", ambayo inatarajia viongozi wa nchi mbalimbali na wajumbe wote kuchangia mawazo kuhusu hali hiyo. Lakini rais Donald Trump wa Marekani anapinga kaulimbiu hiyo hadharani.

    Kwenye mjadala wa kawaida wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa, rais Tump ametetea sera ya "Marekani Kwanza" na kukosoa kamati ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa, mahakama ya kimataifa ya uhalifu na makubaliano ya nyuklia ya Iran, huku akizilaumu Iran, Venezuela, Ujerumani na kueleza wazi wazo la kupinga utandawazi. Hotuba ya rais Trump imelaaniwa na kupingwa na wajumbe wa nchi nyingine.

    Gazeti la Uingereza FT limesema, kwa wale wanaoamini ushirikiano wa kimataifa, mkutano kuu wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa ni fursa ya kujitolea na kulinda ushirikiano wa kimataifa. Marekani ilikuwa mjenzi na mshiriki mkuu wa utaratibu wa uchumi wa dunia na mfumo wa biashara wa pande nyingi baada ya vita ya pili ya dunia, lakini baada ya miaka 70, serikali ya Marekani ya awamu hii inatumia kisingizio cha "Marekani Kwanza" kujitoa kwenye mpango wa uhusiano wa nchi za pasifiki TPP, makubaliano ya hali ya hewa ya Paris, makubaliano ya nyuklia ya Iran, mashirika ya UNESCO na UNHRC, huku ikianzisha vita ya kibiashara kote duniani kupitia njia ya kuongeza ushuru. Bila shaka Marekani imefanya shambulizi kali dhidi ya mfumo wa pande nyingi na katiba ya Umoja wa Mataifa iliyoshiriki kuiunda, na kuleta kizuizi kikubwa kwa maendeleo ya jamii ya binadamu. Kitendo cha Marekani kitapingwa na kuzuiwa na nguvu ya dunia nzima.

    Umoja wa Mataifa ni jukwaa kuu la kutekeleza mfumo wa pande nyingi, ambao si njia ya kutangaza hatua za upande mmoja. Ingawa siasa za umwamba bado zipo duniani, lakini sauti kuu ya jumuiya ya kimataifa ni kuhimiza utaratibu wa kimataifa kuelekea upande wenye haki na usawa na kutimiza ushirikiano wa kunufaishana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako