• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mawaziri wa mambo ya nje wa Marekani na Uingereza wahimiza kuanzishwa kwa kamati ya katiba ya Syria

    (GMT+08:00) 2018-09-28 16:55:42

    Mawaziri wa mambo ya nje wa Marekani, Uingereza, Saudi Arabia na nchi nyingine wametoa taarifa ya pamoja ya kuhimiza ofisi ya mjumbe maalum inayoshughulikia suala la Syria kuanzisha kamati ya katiba ya Syria haraka iwezekanavyo na kuanza kuandaa katiba mpya ya Syria.

    Taarifa hiyo imesema kuwa migogoro ya Syria imeendelea kwa zaidi ya miaka saba sasa, na kusababisha vifo vya mamia elfu na mamilioni ya watu kuyakimbia makazi yao . Ni lazima kumaliza mgogoro kupitia hatua ya kidiplomasia iliyoratibiwa. Taarifa hiyo pia imesema kwa sauti ya nguvu zaidi kuwa kujaribu kutatua suala la Syria kwa njia ya kijeshi kunaweza tu kuimarisha mvutano na kupanua wigo wa mgogoro huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako