• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali ya Zimbabwe kuanza kutoa chanjo ya kipindupindu

    (GMT+08:00) 2018-09-28 18:56:52

    Naibu waziri wa afya na huduma kwa watoto wa Zimbabwe Bw. John Mangwiro amesema serikali imefanikiwa kupata dozi 500,000 za chanjo ya ugonjwa wa kipindupindu ambazo zitaanza kugawiwa wiki ijayo kwa vikundi vilivyo kwenye hatari ya kupata ugonjwa huo.

    Katika wiki tatu zilizopita, takribani watu 49 wamefariki, hasa kitovu chake ikiwa ni kwenye kitongoji kimoja kilichopo kusini magharibi mwa mji mkuu wa Harare.

    Akizungumza na gazeti la the Herald, naibu waziri huyo amesema dozi hizo ni msaada kutoka asasi mbili ambazo ni Benki ya Stanbic, pamoja na Mamlaka ya posta na mawasiliano, ambapo amethibitisha kuwa maandalizi kwa ajili ya kutoa chanjo yamekamilika.

    Aidha serikali ya Zimbabwe imetoa tahadhari kwa idara za kiafya katika majimbo na miji yote kuhusu kutokea kwa ugonjwa huo na kwamba zijiandae kukabiliana nao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako