• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Takribani watu 410 wamefariki nchini Indonesia kufuatia tetemeko Kubwa la ardhi pamoja na tsunami

    (GMT+08:00) 2018-09-29 19:46:37

    Msemaji wa Idara ya kukabiliana na majanga ya Indonesia, Sutopo Purwo Nugroho ametangaza kuwa, takribani watu 410 wamefariki na wengine 540 wakijeruhiwa kutokana na tetemeko kubwa la ardhi lililofuatiwa na tsunami lililotokea kwenye jimbo la Sulawesi katikati ya nchi hiyo.

    Bw. Nugroho amesema waathirika wote wa tukio hilo walipelekwa hospitali, huku akiwaeleza waandishi wa habari kuwa huenda idadi ya vifo na majeruhi ikaongezeka kutokana na janga hilo.

    Kwa mujibu wa mamlaka ya hali ya hewa na mipaka ya Indonesia, maeneo yalioathirika ni kuanzia sehemu za ufukwe wa Talissa katika wilaya ya Dongala, mji wa ufukweni wa Palu, na makao makuu ya jimbo la hilo la Sulawesi.

    Aidha kutokana na tetemeko pamoja na tsunami, watu wengi waliangukiwa na majengo yaliyokuwa yanaporomoka, akisema pia majengo mengi na makazi ya watu viliharibiwa, na kwamba mpaka sasa takwimu kamili za uharibifu huo haijulikani na tathmini inaendelea.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako