• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China atoa rambirambi kwa vifo kutokana na tetemeko pamoja na tsunami nchini Indonesia

    (GMT+08:00) 2018-09-30 19:23:51

    Rais Xi Jinping wa China leo ametoa salamu za rambirambi kwa mwenzake wa Indonesia Bw. Joko Widodo kwa vifo vya watu kutokana na tetemeko la ardhi pamoja na tsunami nchini humo.

    Msemaji wa Idara ya kitaifa inayoshughulikia majanga ya Indonesia Bw. Sutopo Purwo Nugroho amesema vifo kutokana na mfululizo wa matetemeko ya ardhi yaliyopelekea kutokea tsumani lililoharibu jimbo la Sulawesi, vimeongezeka na kufikia 832 na watu 540 wamejeruhiwa na wengine 16,732 wakilazimika kuyakimbia makazi yao.

    Aidha, msemaji huyo amesema idadi ya vifo inaweza kuongezeka wakati huu ambapo tathmini ya uaharibifu ikiendelea, akiamini kuwa bado kuna miili ambayo imefukiwa chini ya kifusi na kwamba shughuli za kuitafuta na uokoaji zinaendelea.

    Wakati huo huo, Rais wa Indonesia Joko Widodo amewasili katika mji wa Palu ambao pia umeharibiwa vibaya, akihimiza jitihada Zaidi kwenye shughuli za uokoaji, na licha uharibifu katika mji wa Palu, uwanja wake wa ndege umefunguliwa kwa ajili ya ndege za uokozi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako