• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wanaharakati wa Kenya watoa mwito wa kuimarisha ulinzi wa wazee

    (GMT+08:00) 2018-10-01 08:52:15

    Wanaharakati nchini Kenya wameitaka serikali kufanya mabadiliko ya sera ili kuwanusuru wazee kutokana na umaskini, kukosa makazi, ujinga, magonjwa na kutengwa na jamii.

    Wakiongea kabla ya siku ya kimataifa ya wazee, wanaharakati hao wamesema kuhimiza kuwepo kwa hali nzuri kwa wazee wanaozidi kuongezeka nchini Kenya kupitia kuboresha mipango ya matunzo ya kijamii, ni sehemu muhimu ya kufanikisha maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya Kenya.

    Leo Kenya itaadhimisha siku ya kimataifa ya wazee, na shughuli za maadhimisho ya kitaifa zinafanyika katika kaunti ya Bomet, ambako viongozi wa Kenya wanatarajiwa kukumbusha dhamira ya serikali kuhimiza matunzo kwa wazee.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako