• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waasi wa Houthi wa Yemen washambulia uwanja wa ndege wa Dubai na bandari ya Saudi Arabia

    (GMT+08:00) 2018-10-01 08:54:34

    Waasi wa kundi la Shia la Houthi wamefanya mashambulizi mawili tofauti ya kuvuka mpaka dhidi ya Umoja wa Falme za Kiarabu na Saudi Arabia.

    Kwa mujibu wa taarifa ya Shirika la habari la Saba linalodhibitiwa na waasi, shambulizi la kwanza lilitekelezwa na ndege isiyo na rubani katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Dubai, na shambulizi la pili lilifanywa na vikosi vya majini vya waasi dhidi ya boti za jeshi zilizokuwa zikiongozwa na askari wa Saudi Arabia mjini Jazan, katika Bahari Nyekundu ya Saudi Arabia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako