• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mji wa Xuzhou watunukiwa Tuzo ya UN-Habitat ya mwaka 2018

    (GMT+08:00) 2018-10-02 09:39:00

          

    Sherehe ya utoaji wa "Tuzo ya Shirika la Makazi la Umoja wa Mataifa UN-HABITAT" ilifanyika jana ambayo ilikuwa Siku ya Makazi ya Duniani kwenye makao makuu ya UN-Habitat mjini Nairobi, Kenya, na mji wa Xuzhou wa China ni moja ya washindi wa tuzo hiyo.

    "Tuzo ya UN-Habitat" ambayo ni tuzo ya ngazi ya juu zaidi katika sekta ya makazi duniani iliyozinduliwa mwaka 1989 na shirika la UN-Habibat, inatolewa kwa serikali, mashirika pamoja na watu binafsi wanaochangia katika kuboresha mazingira ya makazi ya binadamu na kufuatiliwa sana na serikali za nchi mbalimbali duniani. Tuzo tano huandaliwa kila mwaka, na Xuzhou ni mji pekee uliopewa na tuzo hiyo kwa mwaka huu.

    Mji wa Xuzhou ulioko mashariki mwa China ni kituo muhimu cha uzalishaji wa makaa ya mawe. Katika miaka ya hivi karibuni umekuwa ukifanya juhudi kubwa katika kubadilisha njia ya kuzalisha, kushughulikia taka ngumu, na matumizi ya nishati endelevu. Hadi sasa miji 19 na watu wanne nchini China wamepewa tuzo hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako