• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Taifa Stars yaanza kambi kuiwinda Cape Verde

    (GMT+08:00) 2018-10-02 10:12:07

    Kambi ya timu ya Taifa ya Tanzania "Taifa Stars" imeanza rasmi jana kujiandaa na mchezo wa kufuzu kucheza fainali za Africa mwakani dhidi ya Cape Verde.

    Kambi hiyo imeanza na wachezaji wanaocheza ndani kabla ya kuungana na wale wanaocheza nje ya nchi.

    Mazoezi hayo yanafanyika katika viwanja vya kituo cha Jakaya Kikwete mjini Dar es Salaam chini ya kocha mkuu Emmanuel Amunike akisaidiwa na Hemed Morocco na Emeka Amadi.

    Mchezo wa kwanza utachezwa Oktoba 12, 2018 kwenye mji wa Praia huko Cape Verde na mchezo wa marudiano utachezwa Oktoba 16, 2018 Uwanja wa Taifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako