• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Soka, Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya: Mechi za raundi ya pili makundi kupigwa leo usiku

    (GMT+08:00) 2018-10-02 10:13:52

    Ligi ya klabu bingwa barani Ulaya inaendelea leo kwa mechi za raundi ya pili ya hatua ya makundi, ambapo michezo nane itapigwa.

    Kutoka kundi E, AEK Athens ya Ubelgiji itacheza dhidi ya Benfica ya Ureno wakati Bayern Munich itakuwa nyumbani Ujerumani kuikaribisha Ajax ya Uholanzi.

    Kunako kundi F, Hoffenheim ya Ujerumani itakutana na Manchester City ya Uingereza, Lyon ya Ufaransa itacheza na Shakthar Donetsk ya Ukraine.

    CSKA Moscow ya Urusi itapambana na Real Madrid ya Hispania, na AS Roma ya Italia itakuwa kibaruani dhidi ya Viktoria Plizen ya Jamhuri ya Czech, hili ni kundi G.

    Na kwenye kundi H, Juventus ya Italia itacheza na Young Boys ya Uswis, na Manchester United itawakaribisha nchini Uingereza Valencia kutoka Hispania.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako